Waziri mwenye dhamana ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, ameongoza kikao cha wakuu wa vitengo wa sekta ya maendeleo ya jamii kilicholenga kutathmini utendaji wa sekta hiyo na kuweka mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika mkoani Morogoro Dkt. Gwajima amewataka maafisa wa maendeleo ya jamii kukaa katika nafasi zao wakati huu wakuelekea kwenye Dira ya 2050 na kutaka watu wajiamini na kuona fursa ili kuweza kufikia malengo.

Naye katibu mkuu mtendaji Eriak mmbaso amesema kusudi la kukutana katika kikao hicho ni kuhakikisha wanapeana misimamo ya utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2050 kwani jamii inapaswa kubadilika ili kuhakikisha malengo yanafikiwa kwani bila mabadiliko dira haiwezi kubadilika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wakuu wa vitengo wa maendeleo ya jamii nchini Heris Simonile amesema sekta ya maendeleo ya jamii inahusika na kuijenga nchi kwa kuielimisha jamii na kujenga fikra chanya ya jamii ili kuwa wazalendo wa Taifa lao.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *