Onyo hilo limetolewa na Ashwini K.P., Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu aina za sasa za ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kikabila, chuki dhidi ya wageni na aina nyingine za kutovumiliana, wakati akiwasilisha ripoti yake mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi.

Ashwini amesema “Michezo ina nguvu ya kukuza ujumuishi, usawa na mshikamano wa kijamii, lakini bado inaendeleza mifumo ya ubaguzi wa rangi inayoshuhudiwa katika jamii kwa ujumla,” amesema.

Ripoti yake inaonesha kuwa umasikini, migogoro, sera kandamizi na ukosefu wa uwakilishi vinaendelea kuzuia makundi yaliyotengwa kushiriki kikamilifu katika michezo.

“Fursa ya kushiriki michezo bado si sawa kwa wote. Ukosefu wa usawa wa kiuchumi unaotokana na historia ya ubaguzi unaathiri zaidi makundi yaliyotengwa,” amesisitiza.

Amevitaka vyombo vya michezo na serikali kuchukua hatua za dhati kukomesha ubaguzi huo.

“Ni lazima tushughulikie chanzo cha tatizo, ikiwemo mifumo ya kihistoria ya ubaguzi na kutengwa, ili michezo iwe chombo cha kweli cha usawa na haki,” amesema.

Tags: Ubaguzi, michezo, kutovumiliana

Partner: OHCHR

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *