Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women inaonya kuwa si kila maudhui mtandaoni ni mabaya, lakini baadhi ya maudhui hujificha kama ushauri wa kawaida huku yakikuza chuki dhidi ya wanawake, shinikizo la “kuwa mwanaume kamili”, au mtazamo wa ushindani usio na afya.

Dalili za kuangalia

Mzazi au mlezi anaweza kuona mabadiliko haya kwa mvulana:

• Kujitenga zaidi na familia au marafiki
• Kutumia muda mwingi kupita kiasi mtandaoni
• Kutumia maneno kama mimi ni “alpha”, “beta”, au “red pill”
• Kuonesha hasira au mtazamo hasi dhidi ya wanawake

© UN Women/Poompat Watanasiriku Kuzungumza na vijana kuhusu hali ya maisha na usalama mtandaoni – mwongozo kwa wazazi na walezi.

Wazazi/ Walezi wafanye nini?

1. Anza kwa mazungumzo, si hukumu
Muulize kwa utulivu:

  • Unapenda nini kuhusu maudhui hayo?
  • Kitu gani kinakuvutia hapa?

2. Msaidie kufikiri kwa kina
Mfundishe kujiuliza:

  • Ujumbe gani umepata kutoka katika maudhui hayo?
  • Je maudhui hayo ni kweli au ni propaganda?
  • Mtengeneza maudhui huyu anafaidika vipi?

3. Tengeneza mazingira salama ya kuzungumza
Wavulana wengi hufundishwa kuficha hisia zao. Wasaidie kuona kuwa kuomba msaada si udhaifu.

4. Wape njia mbadala nzuri
Michezo, Nafasi ya kuwa mbunifu , Washauri ( Mentors), Watu ambaye ni mfano wa kuigwa (role models) wazuri, hii inaweza kuwasaidia kujenga kujiamini kwa njia yenye afya.

© UN Women/Poompat Watanasiriku Kuzungumza na vijana kuhusu hali ya maisha ulimwenguni na usalama mtandaoni – mwongozo kwa wazazi na walezi.

Kwa nini hii ni muhimu?

UN Women inasisitiza kuwa maudhui mabaya  mtandaoni hayaishii kwenye rununu pekee. Yanaweza kuathiri namna vijana wanavyoongea, kufikiri na kuwatendea wengine katika maisha halisi.

Ujumbe mkubwa ni huu: mazungumzo ya wazi nyumbani yanaweza kuwa kinga muhimu zaidi dhidi ya ushawishi hasi wa mtandaoni.

Soma zaidi kuhusu makala hiyo hapa: UN Women Explainer on the Manosphere 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *