
Wakati huohuo, imebainika kuwa maafisa wakuu wa Marekani waliendesha kampeni kali katika siku tano zilizopita, wakijaribu kuyazuia mataifa kushiriki katika hafla za mazishi ya Ayatullah Khamenei.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim likinukuu chanzo cha ngazi ya juu cha Iran, kampeni hiyo iliratibiwa “katika ngazi za juu” na ilihusisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio pamoja na mabalozi wa Marekani duniani, na ilijumuisha vitisho vya kukatiza misaada ya maendeleo na kuathiri uhusiano wa nchi husika na Washington iwapo zingetuma wajumbe Tehran.
Wanadiplomasia wawili Waarabu, waliyonukuliwa bila kutajwa majina, wamethibutisha kuwa Rubio aliwasiliana binafsi na wenzake katika angalau nchi tano za Kiarabu, akiwahimiza kutojitokeza.
Ripoti hiyo pia imebaini kuwa baadhi ya mabalozi wa Marekani katika mataifa ya Afrika walienda mbali zaidi kwa kutishia wazi kukata misaada ya maendeleo endapo nchi hizo zingetuma wawakilishi Tehran.
Kutokana na shinikizo hilo, ripoti imefichua kuwa angalau nchi 13, ikiwemo nchi tatu za Ulaya Mashariki, nchi tano za Afrika, nchi mbili za Kiarabu za Ghuba ya Uajami, na mataifa mawili makubwa ya Asia ya Mashariki, zilijiondoa katika kushiriki kwenye mazishi.
Baadhi ya nchi hizi zilituma jumbe za kuomba radhi kupitia wapatanishi au misheni za kidiplomasia zilizoko Geneva na New York, zikijaribu kuhalalisha uamuzi wao huo. Nyingine zilijaribu kuteua wanadiplomasia wa ngazi ya chini walioko Tehran ili kuhudhuria, hata hivyo, Iran ilikataa kukubali uwepo wao katika hafla hiyo.”
Licha ya jitihada zote za Washington, wajumbe kutoka zaidi ya nchi 100 walijitokeza kushiriki katika hafla ya mazishi. Hii ni dhihirisho tosha la heshima ya kimataifa aliyokuwa nayo Kiongozi Shahidi, na kwa upande mwingine, ni alama ya kushindwa dhahiri kwa mbinu za shinikizo la kidiplomasia za Marekani dhidi ya mataifa mengine