Chanzo cha picha, NurPhoto via Getty Images
Marekani imewaondoa wanajeshi wake waliopelekwa nchini Nigeria mapema mwaka huu
katika juhudi za kusaidia kupambana na makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali
za kidini.
Mnamo
Desembam waka jana, vikosi vya Marekani na Nigeria vilianzisha operesheni ya
pamoja katika eneo la Bonde la Ziwa Chad, ambayo ilihusisha mashambulizi dhidi
ya wanamgambo siku ya Krismasi, na kufuatiwa na kutumwa kwa wanajeshi 200 miezi
miwili baadaye.
Kiongozi mkuu wa Islamic State (IS)
Abu-Bilal al-Minuki aliuawa wakati wa operesheni hiyo iliyodumu kwa miezi
kadhaa.
Siku ya Alhamisi, Marekani iliangazia
mafanikio yaliyofikiwa katika operesheni hiyo, huku msemaji wa jeshi la Nigeria
akiiambia BBC kuwa kujiondoa kwa wanajeshi wa Marekani “hakutaathiri kasi
yetu kwa vyovyote vile”.
Licha ya oparesheni hizo, makundi ya kijihadi
yameendelea na mashambulizi hasa katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa
Nigeria.
Meja Jenerali Michael Onoja alisema
ushirikiano wa kijasusi kati ya nchi hizo mbili utaendelea, jambo ambalo jeshi
la Marekani pia lilisema katika mkutano wake.
Ushirikiano wa kijeshi kati ya Nigeria na
Marekani uliongezeka baada ya Washington kushutumu mamlaka ya Nigeria kwa kushindwa
kuwakabili vilivyo wapiganaji wa kijihadi, na kudai kulikuwa na “mauaji ya
kimbari dhidi ya waumini wa Kikristo” nchini humo.
Nigeria imekanusha madai hayo, ikisema
ghasia hizo zinaathiri watu kutoka jamii zote.