Dar es Salaam. Wataalamu wa afya nchini wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kutoa elimu sahihi kwa wananchi na kutowaachia watu wasio na utaalamu, kuendelea kusambaza taarifa zinazoweza kupotosha kuhusu masuala ya afya.

Agizo hilo limetolewa leo Jumamosi, Julai 4, 2026 na Naibu Waziri wa Afya, Dk Florence Samizi wakati akizungumza na walimu, viongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Mucohas) kwenye ziara yake ya kikazi chuoni hapo.

Amewataka walimu na wataalamu wa afya kuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu magonjwa mbalimbali, hususan yasiyoambukiza na homa ya ini (Hepatitis), kwa kutumia majukwaa ya kidijitali kama TikTok, Instagram na Facebook.

“Msikae kimya wakati watu wasio wa-taalamu wanatoa taarifa zisizo sahihi. Elimu mliyoipata inapaswa kuisaidia jamii na kuokoa maisha ya Watanza-nia,” amesema.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Florence Samizi akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Julieth Magandi

Kuhusu uzalishaji wa dawa, Dk Samizi amesema kwa sasa asilimia kubwa ya dawa zinazotumika nchini bado zinaagizwa kutoka nje, hali inayohitaji kubadilishwa kupitia uwekezaji wa ndani.

Amesema Serikali tayari imeweka maz-ingira ya kuvutia wawekezaji, ikiwamo kutenga eneo maalumu kwa ajili ya viwanda vya dawa na kupokea maombi ya uwekezaji kutoka mataifa mbalimbali.

Amewataka viongozi wa chuo hicho kutumia fursa ya kuwa na kozi za famasia kuanzisha miradi ya uzalishaji wa dawa na bidhaa nyingine za afya, akisema hatua hiyo itasaidia kuongeza ajira kwa wahitimu, kuongeza mapato ya taasisi na kuchangia azma ya taifa ya kujitegemea katika sekta ya dawa.

“Ninyi mna wataalamu, mna ardhi na mna taasisi yenye historia na kuaminika. Angalieni fursa zilizopo na mshirikiane na wawekezaji ili muanze kuzalisha dawa hapa nchini,” amesema.

Baadhi ya wanafunzi wa fani ya uuguzi na ukunga kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUCOHAS

Katika hatua nyingine, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta ya afya kupitia uwekezaji wa vi-faatiba, ajira za watumishi, uboreshaji wa masilahi na miundombinu ya ku-tolea huduma.

Amesema miongoni mwa mafanikio hayo ni ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na tiba ambavyo hapo awali vilikuwa vinapatikana katika nchi chache duniani, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watumishi wa afya na kutambuliwa kwa sifa za kitaaluma za kada mbalimbali.

“Haya yote yanaonesha namna am-bavyo Rais Dk Samia anaithamini sekta ya afya na anaendelea kuwekeza katika kuboresha huduma kwa wananchi,” amesema.

Dk Samizi amewapongeza walimu wa chuo hicho kwa kuendelea kutoa ma-funzo yenye ubora, akisema matokeo mazuri ya ufaulu wa wanafunzi na kupata ithibati ya programu za maso-mo vinaonesha

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hos-pitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Julieth Magandi, amesema MNH inaendelea kuhakikisha wanafunzi wa fani mbalimbali za afya wanapata ma-funzo ya vitendo yenye ubora katika mazingira yanayowawezesha kujenga umahiri, weledi na maadili ya taalu-ma, ili wahitimu wawe tayari kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.

Naye Mkuu wa Mucohas, Dk Bonny Betson, amesema chuo hicho ki-taendelea kuimarisha ubora wa ma-funzo, tafiti na ubunifu ili kuzalisha wataalamu wenye umahiri, maadili na uwezo wa kukabiliana na changamoto za sekta ya afya nchini na kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *