Msoffe, amesema kuwa mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yatategemea kwa kiwango kikubwa ushiriki wa sekta binafsi, hususan katika kuimarisha mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo na biashara.
Akiongea wawaandishi wa habari katika viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya biashara sabasaba amesema sekta binafsi itachangia zaidi ya asilimi 70 katika mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uthibiti wa Nafaka na Mazao mchanganyiko COPRA Irene Mlola amesema yapo mafanikio makubwa kwenye sekta ya kilimo kimataifa baada ya uwepo wa COPRA.
Aidha mkurugenzi wa fedha na utawala COASCO CPA Sipila Mushi amezita taasisi za serikali ,watu binafsi na mashirika kupata huduma za kishauri wa kitaalam wa kodi ,uongozi na ukaguzi wa hesabu COASCO .
Gooluck Luanjo ni Afisa Mwandamizi kitengo cha TEHAMA kutoka wa soko la bidhaa Tanzania TMX amesema kutokana na kusimamia vema soko la bidhaa kwenye kilimo na madini ya vito sasa wapo kwenye hatua nzuri katika kuanzisha soko la kidital kwenye mifugo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu kutoka Hazina Sacos Dkt Festo Mwaipaja amesema Hazina Sacos inajivunia kwa kuwa na wananchama wengi huku wakimiliki mali zenye thamani ya bilioni 55.8 .
(Feed generated with FetchRSS)