Muandamanaji

Chanzo cha picha, EPA

Nigeria imesema kuwa raia wake wawili wameuawa nchini Afrika Kusini “wakati ambapo raia wa kigeni wanaendelea kulengwa isivyo haki” nchini humo.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria ilisema kuwa Emeka Charles Iroegbu aliuawa tarehe 28 Juni, akidaiwa kufariki mikononi mwa maafisa wa polisi waliotumia “mbinu za kikatili za mahojiano”. Pia ilisema kuwa mmiliki wa duka, Musa Yunana Joe, aliuawa siku hiyo hiyo na watu wasiojulikana.

Hadi sasa, mamlaka za mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, hazijatoa tamko kuhusu matukio hayo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria ilisema kuwa matukio haya yanatokea wakati ambapo hisia za kupinga wahamiaji zinaongezeka nchini Afrika Kusini.

Hali hiyo imesababisha takribani raia 25,000 kutoka mataifa mengine ya Afrika kurejeshwa katika nchi zao, wakiwemo takribani Wanigeria 700.

Waandamanaji nchini Afrika Kusini wamekuwa wakiiomba serikali kuchukua hatua zaidi kudhibiti uhamiaji haramu. Wanasema kuwa raia wa kigeni wanachukua nafasi za ajira na kunufaika isivyo haki na huduma za umma.

Nigeria pia imesema itadai fidia kutoka kwa Afrika Kusini kwa raia wake walioondoka nchini humo, ikiongeza kuwa serikali ya Abuja imeanza kuorodhesha biashara na mali zilizotelekezwa na Wanigeria.

Hata hivyo, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ijumaa, Waziri wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Kusini, Khumbudzo Ntshavheni, alisema serikali yake haitalipa fidia na kwamba Wanigeria wanaweza kuuza mali zao zilizosajiliwa walizoacha nchini humo katika soko la Afrika Kusini.

Unaweza kusoma;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *