Baadhi ya raia wa Tanzania wanaotamani kuandamana hapo kesho kupinga kile wanasema ukandamizaji unaoendelea, sasa wanahofia kufanya hivyo kutokana na vitisho vya serikali pamoja na kumbukumbu mbaya ya mauaji yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Octoba mwaka jana.

Imechapishwa:

Dakika 4 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Polisi wa kutuliza ghasia na askari wengine wenye silaha wameonekana katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, kufuatia wito wa maandamano ya tarehe 7, siku ambayo kawaida huwa ni mapumziko ya sherehe za Saba Saba pamoja na kumbukizi ya kuundwa kwa chama cha African Union of Tanganyika, chama kilichoongoza harakati za uhuru mwaka 1965.

Kwa mujibu wa maofisa waliozungumza na shirika la habari la AFP, wamesema “hii ni doria ya kawaida”, lakini ukweli wa mambo ni kuwa hivi karibuni Serikali ilitangaza tena kusitishwa kwa mikutano ya kisiasa, huku vyombo vya usalama vikitumia majuma kadhaa kutoa onyo kwa raia wanaopanga kuandamana, vikiwataja waandamanaji hao kama ‘wahalifu’.

“Jambo lolote lililofanyika awali la kutumia nguvu kulinda amani lilikuwa ni kionjo tu cha kile kitakachotokea ikiwa watu wataandamana”, alisema mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Walinda usalama wa Tanzania wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Walinda usalama wa Tanzania wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita. REUTERS – Thomas Mukoya

Kauli yake ilikuwa kama ukumbusho wa namna polisi ilitumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji wakati wa maandamano ya uchaguzi uliopita, maandamano yaliyochochewa na kile waandamanaji walidai kuzuiwa kugombea kwa wapinzani pamoja na ongezeko la vitendo vya utekaji na mauaji dhidi ya wakosoaji wa Serikali.

Wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na upinzani, wanasema kuwa vyombo vya usalama viliua maelfu ya raia wakati wa vurugu za uchaguzi, serikali hata hivyo imesema watu 518 pekee ndio waliuawa, bila kusema ni akina nani walihusika na mauaji hayo.

Teresia mwenye miaka 32 alipoteza mdogo wake wakiume, anasema kaka yake alikuwa akifanya kazi ya kuuza nyama kwenye duka lililokuwa kwenye barabara ambayo makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yaligeuka kuwa vurugu.

Samia Suluhu Hassan - Rais wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan – Rais wa Tanzania © AP – Patrick Semansky

Anasema mashuhuda walimwambia kuwa mdogo wake alituhumiwa kushiriki maandamano na kisha kupigwa risasi.

“Naogopa na nimepoteza matumaini kabisa. Sifahamu ni lini mambo yatakuwa mazuri au siku ntakayoona mustakabali mzuri”, alisema Teresia, ambaye alitoa jina la kwanza peke yake kwa kuhofia usalama wake.

Wakati huu ambapo Serikali haioneshi kujutia kwa kilichotokea au kuwajibika kutokana na mauaji yaliyofanyika, Teresia anasema hali ya mambo siku hizi inaogopesha.

“Watu wanaendelea kupotea, kutekwa na hata kuuawa. Hali inaogopesha kwakweli na wengi wetu sisi hatuhisi tuko salama”, aliliambia shirika la habari la AFP.

Kaburi la mtu aiyeuawa katika vurugu za uchaguzi mkuu nchini Tanzania
Kaburi la mtu aiyeuawa katika vurugu za uchaguzi mkuu nchini Tanzania AP

Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani, alionekana na wengi kama mkombozi wa Tanzania, akiondoa makataa ya zuio la mikutano ya vyama vya upinzani na vyombo vya habari, punde tu baada ya kifo cha aliyekuwa mtangulizi wake, hayati John Pombe Magufuli.

Haya hivyo miezi michache baadae, tumaini la demokrasia mpya Tanzania lilitoweka, huku yeye mwenyewe na Serikali yake wakiruhusu vitendo vya ukatili na unyanyasaji mwingine, vitendo ambavyo vinatajwa kuwa vibaya zaidi hata kuliko vilivyofanywa wakati wa mtangulizi wake.

Upinzani nchini Tanzania unaonekana kushangaza na tangazo la karibuni la kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa, ambapo kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesema uamuzi wa serikali ya rais Samia kuzuia mikutano ya kisiasa ni “aibu na kinyume cha katiba, hasa katika wakati ambao alihitajika kutibu taifa”.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Tume ya rais ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman Aprili 23 2026
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Tume ya rais ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman Aprili 23 2026 © ikulumawasliano

Nae naibu mwenyekiti wa chama cha Chadema, John Heche, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa yeye pamoja na timu yake wamekuwa wakilengwa mara kwa mara na Serikali na wanafuatiliwa “magari na askari kanzu wamekuwa wakifuatilia mikutano na misafara yetu usiku na mchana”, alisema Heche.

Chadema hata hivyo kimeshazoea ukandamizaji ambapo wakati huu, mwenyekiti wake wakili Tundu Lissu, anaendelea kusota rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja akikabiliwa na mashtaka ya uhaini, mashataka ambayo yeye mwenye na chama chake wanasema yametengenezwa kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *