Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye ametangaza mwishoni mwa juma kuundwa kwa chama chake cha siasa, hatua inayolenga kuimarisha uhuru wake kutoka kwa Ousmane Sonko.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mpango huu, unaoonekana kama mkakati wa kujizatiti  na unaweza kuwabadilisha mameya katika muungano wake kuwa watu muhimu katika uchaguzi ujao.

Tangazo la Rais Bassirou Diomaye Faye kuhusu kuundwa kwa chama chake cha siasa, lililotolewa mbele ya mkusanyiko mkubwa wa mameya kutoka muungano wake, linafungua awamu mpya katika usawa wa madaraka nchini Senegal.

Bassirou Diomaye Faye - Rais wa Senegal
Bassirou Diomaye Faye – Rais wa Senegal AP Photo/Brian Inganga – Brian Inganga

Mpango huu, uliowasilishwa rasmi kama hatua kuelekea “umoja wa kimfumo” na muundo endelevu wa kambi yake, sasa unatafsiriwa katika duru kadhaa za kisiasa kama mkakati wa kuimarisha uhuru wake polepole dhidi ya mshirika wake wa zamani Ousmane Sonko, kiongozi wa Pastef na sasa rais wa Bunge la Kitaifa.

Katika muktadha ambapo mvutano kati ya viongozi hao wawili wa tawi la utendaji umeongezeka polepole tangu walipoingia madarakani, uamuzi huu unaashiria hatua muhimu katika uundaji upya wa uhusiano wao wa kisiasa.

Ousmane Sonko - Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Senegal
Ousmane Sonko – Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Senegal AP Photo/Misper Apawu – Misper Apawu

Hivi karibuni bunge linaloongozwa na wabunge wengi kutoka chama cha Pastef waliidhinisha mpango wa marekebisho ya katiba, mpango ambao unadaiwa kumzuia rais kuwa mwenyekiti wa chama ambapo dakika chache baada ya hatua hiyo rais Bassirou Diomaye Faye akatangaza kuwa mpango huo utapitia kwenye kura ya maoni.

Hatua hiyo imepingwa vikali na Ousmane Sonko akiitaja kama mbinu hatari ya kisiasa na inaibua maswali kuhusu mienendo ya sasa ya kitaasisi na athari inayowezekana ya kura ya maoni kama hiyo kwenye usawa wa madaraka nchini Senegal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *