Mamilioni ya waombolezaji wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatolla Ali Khamenei jijini Tehran, aliyeuawa miezi kadhaa zilizopita kufuatia mashambulizi ya Marekani nchini humo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakiwa wamefurika katika Barabara kuu za jiji la Tehran, waombolezaji waliovamia mavazi, walionekana wakiangua kilio, mbele ya jeneza la Ayatolla Ali Khamenei lililofunikwa kwa mashada ya maua likipita katika Barabara za jiji hilo.
Mbali na raia wa kawaida, kujitokeza, viongozi waandamizi wa nchi hiyo akiwemo rais wa zamani Mahmoud Ahmadinejad, walitokeza isipokuwa kiongozi mpya wa kiroho Mojtaba Khamenei, mrithi wa Ali Khamenei ambaye aliongoza kwa miaka 40.
Tangu kuchukua nafasi hiyo, Mojtaba ambaye anaelezwa alijeruhiwa vibaya kwenye mashambulizi ya Marekani na Israeli, hajaonekana hadharani.
Baada ya Tehran, wenyeji wa miji ya Qom, Najaf na Karbala, watapata fursa ya kumwomboleza kiongozi huyo siku ya Jumanne na Jumatano, kabla ya kuzikwa kwake siku ya Alhamisi, katika mji alikozaliwa wa Mashhad Kaskazini Mashariki, siku ya Alhamisi.