
Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, ameanza mazungumzo na wanasiasa wa upinzani wa C64 na viongozi wa dini kutoka Jamhuri ya Kidempkrasia ya Congo jijini Gitega, kujadili hali ya kisiasa na usalama nchini humo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mazungumzo hayo yanalenga kutatua sintofahamu ya kisiasa na usalama nchini DRC, wakati huu rais Felix Tshisekedi, akianzisha mchakato wa kuifanyia marekebisho Katiba ya nchi hiyo.
Wanasiasa wa upinzani, wanamtuhumu raus Tshisekedi kuwa, analenga kutumia mabadiliko hayo ya Katiba ili kuwania tena urais mwa muhula wa tatu, wakati muda wake wa kukaa madarakani utakapokuwa umekamilika mwaka 2028.
Ripoti zinasema Donatien N’shole akiwakilisha Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, na André Bokundoa kutoka Makanisa ya Kiprotestanti, yanayopinga mabadiliko ya Katiba wanashiriki kwenye mazungumzo hayo.
Upinzani umeahirisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika wiki hii, kuendelea kupinga marekebisho ya Katiba. Wachambuzu wa siasa wanasema, kwa sababu rais Ndayishimiye ni mshirika wa karibu wa Tshisekedi na kutokana na uelewa wake wa siasa za DRC huenda akawa suluhu ya mvutano wa kisiasa unaoendelea.