Imeelezwa kuwa kasi ya kufikisha umeme kwa kila kitongoji imefikia asilimia 62.

Msimamizi wa Miradi ya REA, Mhandisi, Aneth Malingumu amesema hayo leo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam wakati akieleza mafanikio ya usambazaji umeme vijijini sambamba na kasi ya usambazaji umeme kwenye vitongoji iliyofikiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kufikia sasa.

Mha. Malingumu amesema kuwa, kiwango cha usambazaji wa umeme kwenye vitongoji kimefikia asilimia 62 kati ya vitongoji vyote 64,359 vilivyopo nchini hali itakayosaidia kuboresha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa wananchi kuchochea shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *