Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu imeshuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Serikali ya Qatar inayosimamia huduma za ajira (JUSOUR) na Chama cha Mawakala Binafsi wa Ajira Tanzania (TRAA) kwa ajili ya kuongeza wigo wa fursa za ajira kwa vijana wa Tanzania nchini Qatar.
Wakizungumza baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo Waziri Sangu amesema tangu nchi hizo ziliposaini makubaliano ya ushirikiano wa ajira mwaka 2018 mafanikio makubwa yameonekana katika kuongezeka kwa fursa za ajira kwa Watanzania.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wakala Binafsi wa Ajira (TRAA), Abdallah Mohamed ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea kushirikiana na nchi mbalimbali ikiwemo Qatar na kuongeza kuwa makubaliano waliyosaini na JUSOUR yatawezesha vijana kuomba ajira moja kwa moja huku waajiri kutoka Qatar wakiendelea na uratibu wa usaili na kutoa mikataba yenye maslahi bora kwa waajiriwa.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)