Mamlaka nchini Kenya na Tanzania Jumanne ( Julai 8) zilitumia idara za usalama kama njia ya kuzuia maandamano yaliokuwa yamepangwa kufanyika kuadhimisha siku ya saba saba.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini Kenya ilikuwa imepiga marufuku maandamano ya hapo jana licha ya kuwa walioyapanga walisema walitoa taarifa.

Mkuu wa Polisi jijini Nairobi Issa Mohamud amethibitisha watu 10 walikamatwa kwa kushiriki maandamano hayo na watafikishwa mahakamani hivi leo.

Nchini Tanzania, Polisi na wanajeshi walionekana katika maeneo mbalimbali ya nchi, jiji la kibiashara la Dar es Salaam likisalia mahame kwa sehemu kubwa huku biashara nyingi zilifungwa.

Polisi wakiwa wameimarisha usalama jijini Nairobi wakati wa maandamano ya saba saba.
Polisi wakiwa wameimarisha usalama jijini Nairobi wakati wa maandamano ya saba saba. AP Photo/Andrew Kasuku – Andrew Kasuku

Mataifa hayo jirani ya Afrika Mashariki katika siku za hivi karibuni yamekuwa yakikabiliwa na maandamano dhidi ya serikali, idara zake za usalama zikitumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji, baadhi wakiuawa kwa kupigwa risasi.

Nchini Tanzania, mashirika ya kiraia yanasema watu zaidi ya elfu 1 waliuawa wakati wa maandamano ya wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita, huku nchini Kenya, mashirika hayo yakisema karibia watu 127 waliuawa katika maandamano ya mwaka 2024 na 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *