
Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza rasmi kuwa, katika hatua ya kwanza ya kujibu uchokozi wa Marekani wa usiku wa kuamkia leo, vikosi vya wanamaji na anga vya Jeshi hilo, katika operesheni ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani (drones), vimetekeleza kwa mafanikio mashambulizi makali dhidi ya shabaha 85 muhimu vya kijeshi vya Marekani na kutungua ndege moja ya kisasa ya kijasusi ya adui aina ya MQ9.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Fars, taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano wa Umma cha IRGC imeeleza yafuatayo:
Bismillah Qasim al-Jabbarin (Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwangamizaji wa Madhalimu).
Kufuatia kuleta hamasa kwa taifa kubwa la Iran katika mazishi ya kipekee, yenye kuvunja nguvu ya adui, na makubwa yasiyo na mfano ya kiongozi pekee wa zama hizi na kiongozi shahidi wa Umma wa Kiislamu, utawala vamizi wa Marekani, ambao vipimo vya kushindwa kwake vinazidi kudhihirika siku hadi siku na ambao unachukulia mwamko mkubwa wa kimataifa wa mamilioni ya wananchi wa Iraq katika kumuaga kiongozi huyo shujaa kama pigo kubwa zaidi kwake, umeamua tena kurejea tabia yake ya kuvunja ahadi na, kwa hofu ya kufunika tukio hili la kihistoria, jeshi la kigaidi la Marekani lenye kuua watoto, katika masaa ya mapema ya leo, kwa kushambulia kwa anga idadi ya vituo vya pwani na vituo visivyo vya kijeshi katika fukwe za Mkoa wa Hormozgan na Mahshahr, limevunja waziwazi usitishaji wa mapigano na kukanyaga makubaliano ya Islamabad.
Katika jibu la awali dhidi ya uchokozi huu, vikosi vya wanamaji na anga vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kupitia operesheni ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani, vimefanya mashambulizi dhidi ya maeneo 85 ya vituo muhimu vya kijeshi vya Marekani katika Bandari ya Salman, Eneo la Tano la Wanamaji nchini Bahrain, na Kituo cha Anga cha Ali al-Salem nchini Kuwait, na kutungua ndege moja ya adui aina ya MQ9 iliyokuwa ikikusudia kuingilia operesheni hiyo.
Awali Jeshi la Marekani lilithibitisha mashambulizi ya anga dhidi ya Iran, huku milipuko ikiripotiwa katika maeneo kadhaa ya kusini mwa nchi.
Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) ilidai kuwa mashambulizi hayo yalianza siku ya Jumanne na yalifanywa kama “hatua ya kujibu mashambulizi ya Iran dhidi ya meli tatu za kibiashara zilizokuwa zikipita katika Lango la Bahari la Hormuz.”
Baada ya taarifa hiyo ya CENTCOM, Kamandi Kuu ya Jeshi la Iran, ambayo inajulikana kama Kamandi ya Khatam al-Anbiya ilitoa taarifa ikiahidi kwamba Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu yatatoa “jibu la kusambaratisha” dhidi ya uchokozi huo Marekani.