Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa mikoa ya Morogoro na Tanga kuwa kutakuwa na zoezi la uvutaji waya katika katika njia ya msongo wa kilovoti 33 eneo la Morogoro ili kupisha utekelezaji wa kazi za uvutaji waya (stringing) katika Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma.
Kufuatia zoezi hilo ambalo ni muhimu katika kuhaikikisha Madi wa Chalinze- Dodoma unakamilika ndani ya wakati uliokusudiwa huduma ya umeme itakosekana kwa baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo katika vipindi tofauti, kuanzia tarehe 09 Julai hadi 14 Julai 2026 Ili kuhakikisha kazi hizo zinafanyika kwa usalama.

(Feed generated with FetchRSS)