Aliyekuwa kiongozi wa kiroho wa Ayatollah Ali Khamenei, amezikwa nyumbani kwake katika mji wa Mashhad, unaopatikana Kaskazini Mashariki mwa Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mazishi haya yanafanyika baada ya kushuhudiwa kwa siku kadhaa za maombolezo nchini Iran na nchini Iraq, ambako mamilioni ya watu waliokuwa wamevalia mavazi meusi na picha ya Khamenei, walijitokea kumwomboleza Ayatolla Ali Khamenei, aliyewaongoza kwa miaka 37.

Waombolezaji wameonekana wakiubeba mwili wake kwenye jeneza lililofunikwa kwa bendera ya Iran, huku wakitamka kifo kwa Marekani na Israel.

Waombolezaji wamekuwa wakibeba mabongo yanayosema wanataka kumuuwa Rais Trump
Waombolezaji wamekuwa wakibeba mabongo yanayosema wanataka kumuuwa Rais Trump REUTERS – Alkis Konstantinidis

Ayatolla Khamenei, na baadhi ya wanafamilia wake, waliuawa kufuatia mashambulizi yaliyotekelezwa na Marekani katika makaazi yake jijini Tehran, wakati vita vilipoanza mwezi Februari.

Mrithi wake Mojtaba Khamenei, ambaye ni mtoto wake wa kiume, hajaonekana hadharani kwenye maombolezo ya baba yake, wakati huu kukiwa na ripoti kuwa alijeruhiwa vibaya, wakati wa shambulizi la Februaru 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *