
Serikali ya Eswatini imesema, imewapokea wahamiaji wengine 11 wenye asili ya Afrika, waliofukuzwa kutoka nchini Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wahamiaji hao wamewasili nchini Eswatini siku ya Jumatano, ikiwa ni kundi la nne la watu waliofukuzwa kutoka Marekani kuingia katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.
Mwezi Julai mwaka uliopita, Eswatini ilikubali kuingia kwenye mkataba na Marekani wa Dola Milioni tano, ili kuwapokea wahamiaji 160.
Serikali ya Eswatini imesema wahamiaji hao ni kutoka mataifa ya Afrika, lakini haikuleza utaifa wao.
Mbali na kundi hili la hivi punde, Eswatini tayari imewapokea wahamiaji wengine 19 wote wakiwa wanaume, baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuangiza operesheni dhidi ya wahamiaji wasiokuwa na vibali kuondolewa nchini humo.
Watetezi wa haki za binadamu wakiongozwa na Shirika la Amnesty International, unalaani hatua hii ya Marekani kuwafukuza wahamiaji na kuwapeleka kwenye mataifa ya Afrika.