
Umoja wa mataifa umetoa wito wa kusitishwa mara moja,mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23 ,mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkuu wa tume ya haki katika Umoja wa Mataifa, Volker Turk kwenye taarifa yake amesema inasikitisha kuwa machafuko yanaendelea kuathiri maisha ya raia wa kawaida licha ya kuafikiwa makubaliano kati ya pande hizo hasimu kusitisha vita.
Turk amesema kwa majuma mawili, mapigano yamezidi kati ya pande hizo mbili katika maeneo ya Fizi na Mwengu, mkoa wa Kivu Kusini.
Aidha, UN inasema pande zote mbili zimekuwa zikitumia silaha nzito, droni na vilipuzi katika maeneo yenye wingi wa watu na kusababisha mauaji ,majereha na uharibifu wa makaazi na kuumizwa kwa mifugo.
Machafuko ya hivi karibuni yameripotiwa mapema wiki hii katika kijiji cha Mulima eneo la Fizi.
Kivu Kusini ni baadhi ya maeneo ambayo yameathiriwa pia na mlipuko wa Ebola, hii ikizidisha hali mbaya ya binadaam.