Hali ya utulivu imeshuhudiwa siku ya Ijumaa baada ya siku mbili za mashambulizi mapya kati ya Marekani na Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Utulivu huu wenye mashaka, umejiri wakati huu wasuluhishi wa mzozo huu, ambayo ni nchi ya Qatar ikituma wajumbe wake jijini Tehran kujaribu kuanzisha tena mchakato wa mazungumzo hayo.

Ripoti kutoka Washington nazo zimesema, Marekani ipo tayari kuendelea na mazungumzo ili kupata suluhu ya kudumu baada ya kuzuka tena kwa mashambulizi mapya.

Wakati hayo yakijiri, Iran imesema itajibu mashambulizi ikiwemo kuishambulia Israeli, iwapo miundo mbinu yake itashambuliwa.

Israeli nayo imesema kupitia Waziri wake wa Ulinzi, Israel Katz, kuwa ipo tayari kurejelea tena mashambulizi ya nguvu  nchini Iran, iwapo italazimika kufanya hivyo.

Mashambulizi kati ya Marekani na Iran yalizuka tena wiki hii, kuashiria kuvunjika kwa mkataba wa Juni tarehe 17 wa kusitisha vita, baada ya Washington na Tehran kutuhumiana kuhusu kuanza kushambuliana.

Siku ya Jumatano na Alhamiisi, Marekani ilisema ilishambulia vituo 90 vya kijeshi nchini Iran, huku Iran nayo ikishambulia kambi za kijeshi katika mataifa jirani kama Bahrain.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *