#HABARI: Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Afande Sele, ametumbuiza kwa kishindo katika tamasha la kuadhimisha miaka 30 ya Bongo Fleva linalofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo limewakutanisha kwa mara ya kwanza wasanii wa kizazi cha mwanzo cha Bongo Fleva katika jukwaa moja, wakitoa burudani na kuwakumbusha mashabiki safari ya muziki huo tangu ulipoanza hadi kufikia mafanikio ya sasa.
Mashabiki wamejitokeza kushuhudia tamasha hilo wameonekana kufurahia nyimbo mbalimbali za wasanii hao, huku wakishiriki wakiimba na kushangilia kila msanii alipokuwa jukwaani na kuamsha shamrashamra.
Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva linatarajiwa kuendelea kuwa kumbukizi muhimu katika historia ya muziki wa Tanzania, likiwa na lengo la kutambua mchango wa waanzilishi wa Bongo Fleva na kuenzi urithi wao kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania.
(Feed generated with FetchRSS)