Chanzo cha picha, isna
Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Kigeni wa Iran, Esmail Baghaei, amesema kuwa Tehran haijaomba
kufanya mazungumzo na Marekani, lakini imekubali ombi la mpatanishi mmoja wa
kikanda kutembelea Iran na kujadili matukio yaliyojiri hivi karibuni.
Akizungumza
katika mahojiano ya televisheni, Baghaei alisema kuwa “Hatukuomba kufanya mazungumzo na
Marekani, lakini kwa kuzingatia msimamo wetu wa kuwajibika, hatukukataa ombi la mmoja wa wapatanishi wa
kikanda kuja Iran na kujadili hali ya sasa. Ziara hiyo tayari ilifanyika mjini Mashhad, na tuliwasilisha maoni na misimamo
yetu kwa upande wa Qatar.”
Msemaji huyo aliongezea kuwa “Marekani imekuwa ikikiuka mara kwa mara vipengele
mbalimbali vya makubaliano hayo katika kipindi hiki.”
Baghei alifafanua kuwa
matukio ya Jumatano na Alhamisi yalikuwa ukiukaji wa kifungu cha kwanza na cha
pili cha makubaliano ya
kusitisha mapigano walioafikia na Marekani, huku uamuzi wa kufuta kibali cha
kuuza mafuta ya Iran pia ukiwa ukiukaji mkubwa wa kifungu kingine cha makubaliano hayo.
Kulingana na Baghaei,
kuwekewa kwa Iran vikwazo vipya na Marekani ni kinyume na Kifungu cha 9 cha hati
hiyo ya makubaliano.
Hapo jana Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa Iran imewaomba wafanye mazungumzo ya kupata amani na kutangaza kuwa amefutilia mbali usitishaji mapigano.