Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya sayansi na teknolojia ameusifu ufanisi wa timu ya taifa ya Olympiad ya Hisabati ya Iran baada ya kushinda nafasi ya kwanza katika Mashindano ya Kimataifa ya Hisabati ya China (IMSC) ya mwaka 2026. Mafanikio haya yameelezwa kuwa ni dhihirisho la uwezo wa Iran katika nyanja ya sayansi.

Katika ujumbe wake uliotolewa Jumamosi, Hossein Afshin ameipongeza timu hiyo na kusema: “Kila mafanikio ya kisayansi huenda zaidi ya kupata medali au nafasi katika mashindano; ni ushahidi kwamba rasilimali watu wa Iran, licha ya changamoto zote zinazowakabili, wanaendelea kushiriki na kufanya vyema katika ngazi za juu kabisa za kisayansi.”

Amesemaushindi huu katika mashindano hayo unaonyesha matunda ya miaka mingi ya uwekezaji katika kulea na kuendeleza vipaji vya vijana. Pia amesema ushindi huo umebainisha kuwa Iran inaendelea kuwa miongoni mwa vyanzo vikuu duniani vya vipaji bora vya kisayansi. Aidha, amedokeza kuwa wanafunzi hao wameuonesha ulimwengu taswira halisi ya uwezo wa kisayansi wa Iran kupitia maarifa yao, uvumilivu, na kujiamini kwao.

Afshin amesema serikali ya ina dhamira ya kuendelea kuunga mkono vipaji vya hali ya juu na kuimarisha fursa kwa wasomi wa Iran kushiriki kikamilifu zaidi katika jumuiya ya kimataifa ya sayansi.

Iran imetwaa ubingwa wa timu kwa jumla baada ya kushinda medali nne za dhahabu na mbili za fedha katika mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya timu 49.

Wanachama wa timu ya Iran walioshiriki ni pamoja na Arian Zandi, Arsha Azizoddin, Seyed Amirhossein Tayeb, Alireza Sharifi, Radin Nik-Eghbali, na Ali Joonbakhsh Najafabadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *