Soka la Afrika na dunia limegubikwa na simanzi baada ya kiungo wa Mamelodi Sundowns na timu ya taifa ya Afrika Kusini, Jayden Adams, kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 25.

Adams alikuwa ametoka kuiwakilisha Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026, ambapo alicheza mechi za hatua ya makundi na kuwa sehemu ya kikosi kilichoweka historia kwa kufuzu hatua ya mtoano.

Kifo chake kimethibitishwa na viongozi wa michezo nchini Afrika Kusini pamoja na Chama cha Wachezaji wa Soka cha Afrika Kusini. Hata hivyo, hadi sasa chanzo rasmi cha kifo hakijawekwa wazi, huku mamlaka zikiendelea na uchunguzi.

Jayden Adams ameacha historia ya kuwa mmoja wa viungo wenye kipaji kikubwa nchini Afrika Kusini, alianza kung’ara akiwa Stellenbosch FC kabla ya kuhamia Mamelodi Sundowns, ambako alishinda mataji na kujijengea heshima kubwa.

Kifo chake kimewaacha katika majonzi familia yake, wachezaji wenzake, mashabiki wa soka na wadau mbalimbali duniani.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *