Jumuiya ya Madola imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua ya kuonyesha nia ya maridhiano, mageuzi na uwajibikaji, ikiwamo kuunda tume ya uchunguzi baada ya matukio ya vurugu za Oktoba 29, 2025.

Pia, imeipongeza kwa kuonesha ushirikiano kwa ujumbe wa jumuiya hiyo ulioongozwa na Rais mstaafu wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera, aliyefanya ziara ya siku tisa, Aprili mwaka huu nchini.

Katika ziara yake nchini, Dk Chakwera, alikutana na wadau mbalimbali, wakiwamo viongozi wa vyama vya upinzani na asasi za kiraia.

Pongezi hizo zimetolewa na Kamati ya Mawaziri ya Jumuiya ya Madola (CMAG), baada ya kikao chake cha 73 kilichofanyika Julai 10, 2026.

Pia, kamati hiyo imepokea taarifa ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Serikali, huku ikimtaka Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, kuendelea kushirikiana na Tanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *