
Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, wameanzisha kituo cha kutoa mafunzo ya kukabialiana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Kenya, wakati huu maambukizi zaidi yakiripotiwa nchini DRC.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
MSF wameanzisha kituo hicho nchini Kenya, ili kutoa uwezo kwa wahudumu wa afya kukabiliana na uwezekano wowote wa mlipuko wa Ebola nchini Kenya.
Mafunzo hayo yalianza katikati ya Juni na yanatarajiwa kuendelea hadi Agosti, huku takriban wahudumu 100 wakipatiwa mafunzo kila mwezi. Mbali na wafanyakazi wa MSF, mafunzo hayo pia yatolewa kwa maafisa wa wizara ya afya ya Kenya na mashirika mengine ya misaada.
Shirika la afya kudhibiti magonjwa barani Africa limesema, mlipuko huo ambao ulitangazwa katikati ya mwezi Mei, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 600 na ndio unaokua kwa kasi zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo nchini DRC.
Mlipuko huo umeenea eneo la mashariki ambalo pia linashuhudia utovu wa salama, huku taarifa potofu kuhusu ugonjwa huo zikichangia baadhi ya wananchi kukataa matibabu.
Hadi sasa, wahudumu 112 wa afya wameambukizwa Ebola kati ya visa 1,759 vilivyothibitishwa, na 35 wamefariki dunia.