
Wanajeshi kadhaa wa Nigeria wameuawa wakati wa operesheni ya kuwaokoa wanafunzi 40 waliokuwa wametekwa na watu waliohijami Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la Nigeria limesema operesheni hiyo ilifanyika kwa ushirikiano na vyombo vya ujasusi, polisi na vikundi vya ulinzi wa jamii.
Hata hivyo, limethibitisha kuwa baadhi ya polisi walipoteza maisha au kujeruhiwa wakati wa operesheni hiyo, bila kutaja idadi kamili.
Seneta wa jimbo la Oyo, Abdulfatai Buhari, amesema watoto waliookolewa walionekana dhaifu sana, huku miongoni mwa waliotekwa wakiwa ni watoto wenye umri wa miaka miwili na mitatu.
Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, amesema shambulio hilo lilitekelezwa na wanamgambo wa Ansaru, kundi lililojitenga na Boko Haram.
Utekaji huo ulizua maandamano nchini kote, na kuongeza wasiwasi kuhusu kuenea kwa mashambulizi ya makundi yenye silaha katika maeneo ambayo hapo awali yalionekana kuwa salama, huku Nigeria ikijiandaa kwa uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Januari mwaka 2027.