Hili ni ni agizo jipya lililotolewa na Rais Félix Tshisekedi wakati wa mkutano wa mwisho wa Baraza la Mawaziri mwishoni mwa wiki huko Kinshasa. Tangazo hilo lilitiliwa maanani na mashirika ya kiraia. Je agizo hili ni hatua ya kuelekea mwisho wanajeshi na maafisa polisi kwenye maeneo ya uchimbaji madini?

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Pascal Mulegwa

Kwa Rais wa Jamhuri, uwepo wa wanajeshi na maafisa wa polisi katika maeneo ya uchimbaji madini unakuza ufisadi, Biashara haramu, na mitandao ya uchimbaji madini haramu, huku ukiwakatisha tamaa wawekezaji.

Kwa hivyo, Félix Tshisekedi amewaagiza Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Ulinzi, pamoja na uongozi jeshi na polisi, kuwaondoa mara moja wanajeshi na maafisa wa polisi waliopo katika maeneo ya uchimbaji madini kinyume cha sheria, ili kukomesha kuingiliwa na vikosi vya usalama katika shughuli za uchimbaji madini, na kuwaadhibu wahalifu.

Lakini agizo hili jipya limeacha mahirika ya kiraia yakiwa na mashaka. Timothée Mbuya, wa shirika la Justicia ASBL, anasema kwamba uamuzi kama huo tayari ulifanywa mwaka wa 2019 na kisha tena mwaka wa 2022, lakini haukutekelezwa kamwe. Sababu, anasema, ni kwamba “shughuli hii imekuwa na faida kubwa, wengi wananufaika kabisa. Na mitandao pia imekuwa na nguvu sana.” Kwa sababu mtandao huu haujumuishi tu wanajeshi au maafisa wa polisi; pia unajumuisha wanasiasa na watu wanaojihusisha kisiasa. Kwa hivyo, wanafamilia mashuhuri wanafaidika kutokana na uchimbaji huu wa madini wa ulio kinyume cha sheria, kwa bahati mbaya, wanadumisha mtandao huu. Kinyume na wahusika hawa, kuna wageni wanaofadhili mitandao hii ya mafia kwa mamilioni ya dola za Marekani. “

Mwanaharakati huyo pia anataja kuhusika kwa familia ya rais, ambayo imekuwa ikikanusha mara kwa mara madai hayo. Kwa Justicia ASBL, ni utashi wa kisiasa wa kweli tu katika ngazi za juu za serikali ndio utakaobadilisha uamuzi huu mpya kuwa hatua madhubuti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *