
Mahakama nchini Sudan ,imemhukumu adhabu ya kifo kiongozi wa wapiganaji wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo na ndugu zake wawili ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya Port Sudan inayoshughulikia kesi za ugaidi, adhabu hiyo ikiwahusu Hemetti, ndugu zake Abdelrahim Dagalo na Al-Qoni Hamdan Dagalo pia watu wengi 13 maarufu akiwemo aliyekuwa naibu gavana wa El Tijani AL Tahiri Kashoum na kamanda wa RSF Idris Hassan Haroun.
Mahakama inawatuhumu watu hao 16 kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadaam na mauaji ya kimbari katika mji wa El Geneina, jiji kuu la Darfur Magharibi ambapo gavana wa eneo hilo Khamis Abakar pia aliwauwa Juni 2023.
Aidha mahakama hiyo inamtuhumu Dagalo kwa kupanga uharibifu wa mali za umma na kutumia mbinu za vita zilizoharamishwa.
Mahakama hiyo iliyotoa hukumu hiyo bila watuhumiwa kuwepo mahakamani, imeamuru kutwaliwa kwa mali zote zinazohusishwa na RSF na imeomba kitengo cha kimataifa cha upelelezi Interpol kusaidia kukamatwa na kurejeshwa nyumbani kwa watuhumiwa hao.
Jaji katika mahakama hiyo amesema makosa hayo chini ya uhalifu wa kimataifa haiwezi kusamehewa chini ya mpango wa msamaha wa kisiasa.