
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kisheria na kimataifa, Kazem Gharibabadi, amepinga madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba Tehran na Washington zilifanya mazungumzo kwa saa 11, akisema hakuna mazungumzo yaliyofanyika Oman kati ya maafisa wa Iran na Marekani.
Gharibabadi amesema majadiliano ya ujumbe Iran wakati wa ziara ya hivi karibuni huko Muscat yalijikita katika mikutano na maafisa wa Oman na kwamba hakukuwa na mazungumzo na upande wa Marekani.
“Madai kwamba mazungumzo ya saa 11 yalifanyika baina Iran na Marekani si ya kweli na yanapingwa vikali,” amesema Gharibabadi.
Jumatatu iliyopita, Trump aliimbia Fox News kwamba wapatanishi wa Marekani waliamini kuwa wamefikia makubaliano ya amani ya muda mrefu na Iran kufuatia mkutano wa saa 11 mnamo Julai 12, lakini viongozi wa Iran baadaye walitoa madai mapya.
Akizungumza katika mahojiano ya televisheni Jumanne usiku, afisa huyo wa Iran alisema Tehran ilitaka kuzuia mvutano na Oman kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz na kuwasilisha pendekezo la njia mpya ya usafirishaji.
Akizungumza katika mahojiano ya televisheni Jumanne usiku, afisa huyo wa Iran alisema Tehran ilitaka kuzuia mvutano na Oman kuhusu Lango-Bahari la Hormuz na kuwasilisha pendekezo la njia mpya ya usafirishaji.
Amesema lengo la Iran halikuwa kupinga mamlaka ya Oman kama taifa la pwani mwa Hormuz bali kuhakikisha kwamba njia hiyo ya majini haitumiki kwa njia ambazo zinaweza kutishia usalama wa taifa la Iran.
Akizungumzia kuhusu uchokozi wa Marekani dhidi ya Iran, Gharibabadi ameyataja mashambulizi ya sasa ya Marekani kuwa ni “ya kikatili na uhalifu” na akasema majibu ya Tehran yanapaswa kuzuia mashambulizi ya siku zijazo.
Iran imefunga njia ya maji Lango Bahari la Hormuz ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na uchokozi huo, na kusema njia hiyo ya kiistratijia itaendelea kufungwa hadi Marekani itakapokomesha uhalifu wake.