Iran: Makubaliano na Marekani Hayapo Tena

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema hakuna tena kinachoitwa Makubaliano ya Islamabad kati ya Iran na Marekani, akidai mashambulizi mapya ya Marekani yamefuta kabisa msingi wa maelewano kati ya pande hizo mbili.

Kauli hiyo imekuja baada ya Marekani kufanya mashambulizi mapya kusini mwa Iran na kutangaza kurejesha kizuizi cha majini dhidi ya bandari za Iran.

Kwa kujibu, Iran imesema kupitia IRGC na jeshi lake imelenga vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Kuwait, Bahrain na Jordan kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani.

Mvutano kati ya Iran na Marekani unaendelea kuongezeka, hali inayoongeza wasiwasi wa usalama katika eneo la Mashariki ya Kati.

Je, unaona mgogoro huu unaweza kutatuliwa kwa njia ya diplomasia au utaendelea kuongezeka Tuambie maoni yako kwenye sehemu ya maoni.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *