Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limewasimamisha kwa muda Masheikh wa mikoa ya Dar es Salaam, Singida na Kigoma kwa madai ya mwenendo unaokiuka misingi na taratibu za uongozi.

Uamuzi huo mzito umefikiwa katika kikao cha dharura kilichoongozwa na Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ally Khamisi Ngeruko.��Waliosimamishwa ni Sheikh Walid Alhad Kawambwa (Dar es Salaam), Sheikh Issa Nassor Issa (Singida), pamoja na Sheikh Hassan Kiburwa wa mkoani Kigoma.

Kufuatia hatua hiyo, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dokta Abubakar Zubeir Mbwana, amewateua Sheikh Abasi Ramadhani Abasi, Sheikh Issa Ramadhani Simba na Sheikh Uwesu Mohamed Kiumbe kukaimu nafasi hizo katika mikoa husika ili kuhakikisha huduma na uongozi zinaendelea.

��Mhariri @moseskwindi
#azamtvupdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *