Huduma za upasuaji wa kibingwa zinaendelea kuwafikia wananchi wa Arusha kupitia hospitali inayotembea ya Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyowekwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mgonjwa wa kwanza kufanyiwa upasuaji kupitia huduma hiyo, Arnold Macha, amesema amefanikiwa kuondolewa uvimbe uliokuwa pembeni ya jicho lake tangu mwaka 2020 baada ya kupata huduma hiyo bure.

Ofisa Habari na Mahusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Irene Mbonde, amesema zoezi la utoaji wa huduma linaendelea huku wananchi wakihimizwa kujitokeza kupata huduma mbalimbali za kibingwa zinazotolewa na madaktari bingwa wa hospitali hiyo.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *