Tanzania imeanza kutumia Mobile Operating Theatre ya kwanza Afrika Mashariki, hatua inayotarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma za upasuaji kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Huduma hiyo imeanza kutumika katika kambi ya matibabu bila malipo inayoendelea katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, ambapo wananchi wanapata uchunguzi, matibabu na huduma za upasuaji bila gharama.
Mbunge wa Arusha Mhini, Paul Makonda amesema uwekezaji huo umeongeza uwezo wa kufikisha huduma za kibingwa karibu na wananchi, hususan katika maeneo yenye changamoto ya miundombinu ya afya.
Amesema Mobile Operating Theatre hiyo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha huduma za afya na kuongeza upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi wengi zaidi nchini.
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)