Mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba wenye thamani ya shilingi milioni 400 unatarajiwa kuongeza ajira na uzalishaji wa samaki kwa vijana wa Kata ya Lupingu wilayani Ludewa, mkoani Njombe.

Mradi huo unatekelezwa kupitia Programu ya Taifa ya Uwezeshaji Vijana Kiuchumi ya Shilingi Bilioni 200 kwa lengo la kuwawezesha vijana kutumia rasilimali za uvuvi kujiajiri na kuongeza kipato.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Maendeleo ya Vijana), Joel Nanauka amesema uwekezaji huo umehusisha ujenzi wa vizimba vya kisasa, mafunzo ya kitaalamu pamoja na upatikanaji wa chakula cha samaki ili kuhakikisha uzalishaji wenye tija.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *