Baada ya mkutano na mwenzake wa Marekani, Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz amesema kwamba Israel inataka kudumisha vikosi vyake vilivyowekwa katika “maeneo salama” yaliyoanzishwa Lebanon, Syria na Ukanda wa Gaza.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz alimwambia mwenzake wa Marekani, Pete Hegseth, leo Alhamisi usiku “uamuzi” wa Israel wa kudumisha vikosi vyake vilivyowekwa katika “maeneo salama” yaliyoanzishwa Lebanon, Syria, na Ukanda wa Gaza.

Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel imesema watu hao wawili walizungumza usiku wa kuamkia leo Alhamisi, ambapo waziri “amesisitiza azimio la Israel la kubaki katika maeneo salama nchini Syria, Gaza, na Lebanon ili kulinda mipaka ya Israel na jamii za mpakani kutokana na vitisho vinavyotokana na vikosi vya wanajihadi.”

Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz amesema kwamba vikosi vya Israel vitabaki katika kile alichokielezea kama “maeneo salama” nchini Lebanon, Syria, na Gaza kwa muda usiojulikana, bila ratiba ya kuondoka.

Akizungumza katika sherehe ya ukumbusho wa wanajeshi waliouawa katika vita vya 2006 na Lebanon, Katz alisema: “Jeshi la Israeli litabaki katika maeneo salama nchini Lebanon, Syria, na Gaza hadi itakapotangazwa hatu nyingine tena ili kuwalinda wakazi na jamii zetu kutokana na makundi ya kijihadi.” “Alibainisha kwamba Israel “haitaondoka katika maeneo salama.” Katz pia alirudia onyo lake kwa Tehran, akisema kwamba Iran itakabiliwa na mashambulizi “kwa nguvu zake zote” ikiwa itashambulia vikosi vya Israel vinavyoendesha harakati zake nchini Lebanon.

Matamshi yake yalikuja siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kusema wanajeshi wa Israel watabaki Lebanon mradi tu kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran itaendelea kuwa tishio kwa wakazi wa kaskazini mwa Israel. Viongozi wa Israel wamerudia kusema kwamba jeshi halitaondoka Lebanon hadi Hezbollah itakaponyang’anywa silaha. Mgogoro huo ulienea hadi Lebanon mnamo Machi 2, wakati Hezbollah iliporusha makombora dhidi ya Israel kujibu mauaji ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, siku ya kwanza ya shambulio la pamoja la Marekani na Israel mnamo Februari 28. Israel ilijibu kwa mashambulizi makubwa ya anga na uvamizi wa ardhini kusini mwa Lebanon ulisababisha vifo vya watu 4,300, kulingana na mamlaka ya Lebanon.

Kando na hayo, vyama vya mrengo wa kulia vya Israel na wanasiasa mashuhuri walikaribisha maoni ya Netanyahu siku ya Jumanne, ambapo aliacha wazi uwezekano wa kurejesha makazi ya Israel katika Ukanda wa Gaza, akitaka matamshi haya yatafsiriwe kuwa hatua za vitendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *