Kwa usiku wa tisa mfululizo, wa Jumapili, Julai 19 kuakia Jumatatu, Julai 20, 2026, Marekani imetangaza kuwa imefanya mashambulizi dhidi ya Iran. Tehran imelipiza kisasi tena kwa mashambulizi dhidi ya majirani zake wa Ghuba na kudai kuhusika na shambulio la kombora dhidi ya ndege ya kijeshi ya Marekani katika uwanja wa ndege wa Aqaba wa Jordan, karibu na mpaka na Israel, “na kusababisha uharibifu mkubwa,” kulingana na televisheni ya serikali.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Walinzi wa Mapinduzi wa Iran, walionukuliwa na shirika la habari la FARS, walidai kwamba pia walilenga kambi ya anga ya Ali Al-Salem huko Kuwait.

Siku ya Jumatatu, Julai 19, Walinzi wa Mapinduzi wa Iran wamedai kulenga ndege za kijeshi za Marekani katika uwanja wa ndege wa Aqaba huko Jordan, “na kusababisha uharibifu mkubwa kwa ndege kadhaa,” kulingana na televisheni ya serikali. Ndege nzito za usafiri na doria “za jeshi la Marekani wavamizi” zilishambuliwa na makombora ya balestiki, Walinzi wa Mapinduzi wa Iran wamesema katika taarifa. Siku iliyotangulia, jeshi la Israel, kwa usaidizi wa Jordan, liliripoti kudondosha kombora la Iran lililolenga Aqaba, bandari ya Bahari Nyekundu karibu na Eilat, Israel.

 Huko Kuwait, jeshi liliripoti kukabiliwa na “mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Iran” mapema Jumatatu asubuhi. Walinzi wa Mapinduzi wa Iran walidai kushambulia kambi ya anga ya Ali Al-Salem, kuchoma moto ndege kadhaa zisizo na rubani zilizokuwa hapo, na kuharibu rada ya tahadhari ya mapema ya Marekani. Baada ya hapo, ving’ora vya mashambulizi ya anga pia vilisikika huko Bahrain, kunakopatikana kambi kubwa ya jeshi la majini la Marekani. Ubalozi wa Marekani nchini Bahrain umewaonya raia wake kuhusu mashambulizi yanayowezekana katikati ya mji mkuu, Manama.

Walinzi wa Mapinduzi pia wametangaza kwamba walifanya “shambulio la kushtukiza dhidi ya kituo cha amri maalum ya operesheni za adui katika eneo la Al-Tanf, kama kulipiza kisasi kwa damu ya wanajeshi waliouawa huko Iranshahr,” shirika  la habari la serikali la IRNA limeripoti kwenye Telegram. Jumapili jioni, shirika hili la habari la serikali, Tasnim, lilitaja mazishi ya wanajeshi watatu waliouawa katika shambulio la Marekani kwenye kambi katika mji huu wa kusini mashariki mwa Iran.

Kwa upande wake, Marekani imesema kwamba imeishambulia Iran kwa usiku wa tisa mfululizo siku ya Jumatatu. Mashambulizi hayo “yamelenga vituo vya amri vya kijeshi, maeneo ya ulinzi wa anga na ufuatiliaji wa pwani, uwezo wa baharini, maeneo ya kurusha makombora na ndege zisizo na rubani, na mitandao ya mawasiliano, ili kupunguza zaidi uwezo wa Iran kushambulia meli za kibiashara na mabaharia wa kiraia wanaopitia Mlango wa Hormuz,” Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani (CENTCOM) imesema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *