Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema nchi yake ipo katika “vita kamili” na Marekani.

Pezeshkian amesisitiza kuwa vita vya sasa havihusishi makombora pekee bali pia uchumi na maisha ya wananchi.

Masoud Pezeshkian - Rais wa Iran wakati akitia saini makubaliano kati ya Marekani na Iran.
Masoud Pezeshkian – Rais wa Iran wakati akitia saini makubaliano kati ya Marekani na Iran. via REUTERS – Iran’s Presidential website/WANA

Aidha, amesema Marekani imeshindwa kuilazimisha Iran kujisalimisha kupitia mashambulizi ya kijeshi na sasa inaendesha vita vya mseto vinavyolenga uchumi na ustawi wa wananchi wa Iran.

Katika hatua nyingine, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesema nchi hiyo imepokea mapendekezo kutoka kwa wapatanishi huku mashambulizi ya kulipizana kati ya Tehran na Washington yakiendelea.

Baghaei amesema Iran inaendelea na juhudi za kidiplomasia sambamba na majibu yake ya kijeshi dhidi ya mashambulizi ya Marekani. 

Судна в Ормузькій протоці.
Meli zikiwa kwenye Mlango wa bahari wa Hormuz © Stringer / Reuters

Kuhusu Mlango wa Hormuz, amesema Iran itaendelea kutumia mamlaka yake juu ya njia hiyo muhimu ya maji na kuzuia matumizi yoyote yanayoweza kuhatarisha maslahi yake.

Katika wiki moja iliyopita, Marekani imefanya mashambulizi kadhaa katika kusini mwa Iran, ikisema yanalenga kupunguza uwezo wa Tehran wa kutishia usafirishaji wa kibiashara baharini. Iran nayo imejibu kwa mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani katika nchi  Kuwait, Bahrain na Jordan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *