TIMU ya Mlandege inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar, imefumua kikosi chake baada ya kutangaza kuachana na wachezaji 18 kuelekea msimu ujao wa 2026-2027.

Wachezaji hao ni Abuubakar Hussein Ali, David John Chiwalanga, Fasbir Sabri Ramadhan, Hamad Ubwa Hamad ‘Baro’, Ibrahim Samwel Tuvan, Lucas Sadock Ntikahela, Mussa Hassan Salum na Nonyem Emmanuel Okorocha.

Wengine ni Qassim Nassour Hilal, Ramadhan Mzee Kiparamoto, Said Mussa Said, Said Suleiman Othman, Salum Suleiman Salum, Sospeter Maiko Chikande na Yusuf Jamal Khamis.

Kati ya wachezaji hao, wapo ambao tayari wamejiunga na timu zingine akiwemo Baro aliyetimkia KVZ sambamba na Said Mussa Mbeki, huku Mussa Hassan Simba ‘Mbappe’, ametua Singida Black Stars ya Tanzania Bara na Nonyem Emanuel ‘Okorocha’ aliyepo Pamba Jiji.

Katika taarifa iliyotolewa na Mlandege, iliwatakia kheri wachezaji hao kwa kujitolea kwao kuhakikisha wanaipigania timu katika kila hatua.

“Tunawaaga lakini mtaendelea kubaki sehemu ya familia ya Mlandege, tuna kutakieni kila la kheri na mafanikio mema katika hatua ya mafanikio inayofuata,” ilisema taarifa hiyo.

Mlandege ambayo msimu wa 2024-2025 ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar kisha 2025-2026 ikamaliza nafasi ya nne, imedhamiria kusuka upya kikosi chake ili kurudisha makali msimu ujao wa 2026-2027.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *