.

Chanzo cha picha, viralnigeria

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 5

Alan Reeves alikuwa mmoja wa wachezaji maarufu wa kundi la The Dreamboys nchini Uingereza katika miaka ya 1990. Lakini alipofikisha miaka ya 30, anasema alianza kupoteza hamu ya kufanya ngono, hali iliyomwathiri kihisia na kuleta changamoto katika uhusiano wake wa muda mrefu.

Sasa akiwa na umri wa miaka 52 na akifanya kazi kama mkufunzi wa mazoezi na mtindo wa maisha mjini London, Reeves anasema tiba ya kuongeza homoni ya testosterone imemsaidia kurejesha hamu yake ya kufanya ngono na nguvu za mwili.

“Nilihisi kama nimerejea katika miaka yangu ya ishirini,” anasema.

Si wanaume pekee wanaotumia tiba hiyo.

Rachel Mason, mwenye umri wa miaka 37 na mwandishi wa masuala ya ukomo wa hedhi, anasema matumizi ya testosterone yameboresha nguvu zake na hamu ya kufanya ngono.

Katika mwaka 1990, watu wenye umri wa kati ya miaka 16 na 44 walikuwa wakifanya ngono wastani wa mara tano kwa mwezi.

Kufikia mwaka 2000, wastani huo ulikuwa umeshuka hadi mara nne kwa mwezi, na mwaka 2010 ukafikia mara tatu kwa mwezi.

Matokeo mapya ya utafiti huo yanatarajiwa kutolewa baadaye mwaka huu, huku watafiti wakitarajia mwenendo huo wa kupungua kuendelea, ingawa wanasema bado hakuna sababu moja kwa moja inayoweza kueleza mabadiliko hayo.

Kwanini hamu ya kufanya tendo la ndoa yapungua?

.

Kupungua kwa hamu ya kufanya ngono ni jambo ambalo watafiti wanasema linaonekana kuongezeka katika makundi mbalimbali ya watu.

Soazig Clifton, mkurugenzi wa kitaaluma wa utafiti wa Natsal, anasema tafiti zimeonyesha kupungua kwa kiwango cha watu wanaofanya ngono katika karibu kila kundi la jamii.

Anasema ingawa idadi ya wanandoa wanaoishi pamoja imepungua ikilinganishwa na miaka ya 1990, hata miongoni mwa wanaoishi pamoja, kiwango cha kufanya ngono kimeendelea kushuka.

Kwa mujibu wa Clifton, baadhi ya kupungua kwa kasi zaidi kumeshuhudiwa miongoni mwa wanandoa walio kwenye ndoa au wanaoishi pamoja, hasa wenye umri mkubwa.

Hata hivyo, watafiti wanasema bado hakuna ushahidi wa kutosha unaoweza kueleza kwa uhakika sababu zinazofanya watu wengi siku hizi wawe na hamu ndogo ya kufanya ngono.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ujinsia na usherati ni vipengele tofauti na vilivyojumuishwa katika tendo la ngono la binadamu. Katika kipindi chote cha maisha , imefunzwa na kuainishwa kuhusu raha ya maisha ya kila siku, ya mwili, ya kufurahiana, miongoni mwa wapendanao.

Wazee wana mahitaji sawa ya kutaka kupata raha na ustawi kama watoto, vijana na watu wazima.

Kusalia na hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa katika kipindi cha uzeeni kunapaswa kuwa haki ya kibinadamu na kiashiria muhimu cha ubora wa maisha.

Njia ambayo kila mtu anahisi na kujieleza kama mwanamke au kama mwanamume ni ukweli wa kibayolojia ambao hudumu maisha yote, ndivyo walivyo kijinsia.

Raha haipungui kwasababu ya umri

D

Chanzo cha picha, Getty Images

Wazee wengi husalia kushirikia katika tendo la ndoa hatua inayoashiria kwamba , hamu ya tendo hilo na raha yake haipungui mtu anapozeeka.

IJapokuwa umri pekee haupaswi kuwa sababu ya kubadili viwango vya tendo la ndoa ambavyo vimefurahiwa katika kipindi chote cha maisha , inawezekana kwamba, mazoea inapofaa , kwa mapungufu fulani ya kimwili na madhara ya magonjwa au dawa yanapaswa kuzingatiwa.

Mabadiliko haya yatazungumziwa kwa uchache na hisia zinazohusiana na mhemko huathirika kidogo wakati mtu anaposhiriki tendo la ndoa. Mawazo, msisimko wa hisia, na visaidizi vingine vya kimazingira vinaweza kuongeza uwezo wa kupata raha.

Miongoni mwa wanaume, vipengele vinavyohusiana na kusisimka ndivyo vinavyoshauriwa zaidi, kupitia krimu za juu hadi viungo vya uume. Miongoni mwa wanawake, vipengele vinavyohusiana na ulainishi na vichochezi vya hisia kama vile manukato na nguo za ndani.

Hata hivyo, ni lazima kuzingatia kwamba kuna watu wazima ambao wanachagua kutoshiriki katika shughuli za ngono, na hilo pia ni jambo la kawaida.

Umri na Uzee

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanaume wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuendelea kufurahia maisha ya ngono wanapozeeka kuliko wanawake, kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika British Medical Journal.

Utafiti huo, uliohusisha takriban watu 6,000 nchini Marekani, unaonyesha kuwa mwanaume mwenye umri wa miaka 55 ana wastani wa miaka 15 ya maisha ya ngono yaliyo hai mbele yake, wakati mwanamke wa umri huo ana wastani wa miaka 10 na nusu.

Watafiti wanasema afya njema ndiyo ufunguo, kwa kuwa huongeza hamu ya kufanya ngono na kiwango cha kufurahia tendo hilo.

Kwa mujibu wa utafiti huo, watu wenye afya nzuri wana uwezekano karibu mara mbili zaidi wa kuwa na hamu ya kufanya ngono kuliko wale wenye afya dhaifu.

Pia wana uwezekano mkubwa wa kufanya ngono mara moja au zaidi kwa wiki na kuripoti kuridhishwa zaidi na maisha yao ya ngono.

Kwa ujumla, wanaume walikuwa na uwezekano mkubwa kuliko wanawake wa kuwa bado wanafanya ngono, kuridhishwa na maisha yao ya ngono na kuendelea kuwa na hamu ya kufanya ngono.

Tofauti hiyo iliongezeka kadri umri ulivyoongezeka.

Miongoni mwa wenye umri wa kati ya miaka 75 na 85, asilimia 38.9 ya wanaume walisema bado walikuwa wanafanya ngono, ikilinganishwa na asilimia 16.8 ya wanawake.

Aidha, asilimia 41.2 ya wanaume walisema bado walikuwa na hamu ya kufanya ngono, huku wanawake wakiwa asilimia 11.4 pekee.

Watafiti Stacy Tessler Lindau na Natalia Gavrilova wa Chuo Kikuu cha Chicago wanasema huenda tofauti hizo pia zinachangiwa na uwepo wa mwenza.

Takribani robo tatu ya wanaume katika makundi yote ya umri walisema walikuwa na wenza.

Kwa wanawake, karibu theluthi mbili ya wenye umri wa miaka 25 hadi 54 walikuwa na wenza, lakini kwa wanawake wenye umri wa miaka 75 na zaidi, idadi hiyo ilishuka hadi chini ya wanne kati ya kila 10.

Hali hiyo inaelezwa na ukweli kwamba wanawake huishi kwa muda mrefu zaidi kuliko wanaume na wanaume wengi huoa wanawake wenye umri mdogo kuliko wao.

Akizungumzia matokeo hayo, Profesa Patricia Goodson wa Chuo Kikuu cha Texas A and M alisema ni habari njema kwamba watu wazima wanaweza kufurahia “miaka mingi ya maisha ya ngono hata baada ya kutimiza miaka 55.”

Hata hivyo aliongeza:

“Kipimo hiki hakijatoa mwanga kuhusu swali linalovutia lakini ambalo bado halijaeleweka vizuri. Kwa nini, licha ya kuwa na miaka michache zaidi ya maisha ya ngono, wanawake wengi hawaoni hali hiyo kuwa tatizo?”

Alisema pia:

“Wala hakielezi kwa kina jinsi wanawake na wanaume wanavyokabiliana, wanavyojaribu kuboresha au wanavyokabiliana kwa njia tofauti na mabadiliko ya maisha yao ya ngono wanapozeeka.”

Kwa upande wake, mshauri wa masuala ya mahusiano wa shirika la Relate, Paula Hall, alisema:

“Uwezo wa kufanya ngono hupungua kadri tunavyozeeka.”

Lakini akaongeza:

“Kibiolojia, iwapo watu wana afya njema, hakuna sababu inayowazuia wanandoa kuendelea kuwa na maisha ya ngono.”

Na akahitimisha kwa kusema:

“Sababu inayowafanya watu waache kufanya ngono ni ileile inayowafanya waache kuendesha baiskeli. Ima hawawezi tena kuipanda, au hawana baiskeli.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *