Morogoro. Ofisa ardhi wilaya ya Kilombero, Zakaria Malika (57) ameuawa na watu wasiofahamika baada ya kumvamia nyumbani kwake eneo la kibaoni Ifakara kisha kumshambulia kwa kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibaoni, Saidina Omary amesema tukio hilo limetokea Julai 19 majira ya usiku na kwamba yeye alipata taarifa majira ya saa mbili usiku na baada ya kufika eneo la tukio walikuta mwili wa mtumishi huyo ukiwa umekatwa na kitu chenye ncha kali eneo la nyuma ya kichwa.
“Baada ya kufika hapa kwenye eneo la tukio tuliukuta mwili wa Malika ukiwa umelala chini kifudifudi, ukiwa na majeraha kichwani na maeneo mengine. Tuliwasiliana na wenzetu wa polisi na mara moja walifika na kuchukua mwili kupeleka kuhifadhi hospitali huku tukisubiri taratibu nyingine,” amesema Omary.
Amesema mbali na kuuawa kwa mtumishi huyo, mke wake alipata majeraha kidogo kwenye mkono katika harakati za kujiokoa.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jana Jumatatu, Julai 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Andrew Kantimbo amesema ofisa huyo alivamiwa saa 2:30 na watu ambao idadi yao haijafahamika na kumjeruhi na kitu chenye makali na kusababisha kifo chake.
Wananchi wa Ifakara na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakiwa wamebaba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Afisa ardhi wa wilaya hiyo Zakaria Malika (57) anayedaiwa kuuawa na baada ya kumvamia nyumbani kwake kata ya Kibaoni Ifakara na kukatwa na kitu chenye makali usiku wa kuamkia Julai 20. Picha Hamida Shariff
Kantimbo amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa muda mrefu ya ardhi, uliopo baina ya marehemu na watu wengine.
“Kufuatia tukio hili, Jeshi la Polisi linawashikiliwa watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ambao kwa sasa wanaendelea kuhojiwa,” amesema.
Kamanda Kantimbo amewataka wananchi kutafuta njia sahihi na salama za kutatua migogoro hususani ya ardhi, badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Akitoa salamu za pole wakati wa kuaga mwili wa mtumishi huyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Pilly Kitwana amesema kifo cha Malika kimeacha pengo kubwa kwa halmashauri kwa kuwa alikuwa ni mtumishi wa muda mrefu aliyefanya kazi kama mtaalamu mzoefu kwenye idara ya ardhi.
“Mimi mkurugenzi na watumishi wenzangu wa halmashauri kiukweli tumepata pigo kubwa, kwanza imekuwa ni kifo cha ghafla na cha kikatili, Mzee Malika alikuwa mtumishi msikuvu, mcheshi mwenye nidhamu na bidii ya kazi yake,” amesema Kitwana.
“Alikuwa anamheshimu kila mtu na kila rika, hakika halmashauri tumepoteza nguvu kazi yetu muhimu, lakini ndio kazi ya Mungu, tunamwombea ampumzishe salama,” amesema.
Akieleza taratibu za mazishi, mkurugenzi huyo amesema mwili wa Malika ungesafirishwa jana Juni 20 kwenda kwao Iringa akwa ajili ya maziko leo Jumanne, Julai 21.
Amesema kwa sasa wanaliachia Jeshi la Polisi na mamlaka nyingine ziendelee na uchunguzi, akiwataka watumishi wa halmashauri hiyo kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mtumishi mwenzao.
Vijana hawapaswi kuwa watazamaji kwenye uwekezaji uliofanyika Kibaha, ili Wawekezaji walipe kodi watahitaji vijana wanaofanya kazi ndio maana Serikali ikaamua kujenga vituo hivyo kuwaandaa vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.
Amesema Mkoa wa Pwani umekuwa kiungo cha mkoa wa kibiashara wa Dar es Salam na hivyo uwepo wa karakana hiyo ya kisasa karibu na barabarani kuu itahudumia magari yanayotumia njia hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema moja ya sababu ya wawekezaji kuukimbilia na kuwekeza mkoa humo ni uwepo wa umeme wa uhakika tofauti na miaka yanyuma.
“Mkoa wa Pwani tumeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wetu ndio maana kila kukicha kumekuwa na ongezeko la viwanda ambapo imesaidia katika kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa huu na mapato yetu,” amesema Kunenge.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika ukusanyaji wa kodi jambo ambalo limekuwa na faida kwa Manispaa kwa kutumia fedha kujenga vitega uchumi na kutoa mikopo ya asilimia kumi.
Amesema ujenzi wa vitega uchumi katika Manispaa hiyo utasaidia kuendeleza dira ya 2050 kupitia sekta binafsi na kuinua uchumi katika harakati za kuboresha sekta hiyo.