#HABARI: Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amezindua rasmi mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 33 kutoka Masasi hadi Newala, uliogharimu shilingi bilioni 4.56 kwa umbali wa kilometa 76.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, ameeleza kuwa mradi huo utamaliza kero ya kukatika mara kwa mara kwa umeme wilayani Newala, ambapo awali ilitegemea umeme kutoka Mtwara kupitia Nanyumbu kwa umbali wa kilometa 170.

Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Mwangi Kundya, ameipongeza Serikali kwa kufanikisha usambazaji wa umeme katika vijiji vyote 785 vya mkoa huo pamoja na kutoa vitendea kazi vikiwemo magari 11.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, amebainisha kuwa Mtwara sasa inazalisha zaidi ya megawati 50 za umeme ili kukidhi mahitaji yanayokua kwa kasi mkoani humo na Lindi.

Katika kuelekea kupata suluhu ya kudumu, Waziri Ndejembi amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na mpango wa kuiunganisha mikoa hiyo na Gridi ya Taifa.

Sambamba na hilo, TANESCO imetenga shilingi bilioni 5.27 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kubadilishia umeme (Switching Station) kitakachokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya wananchi na wawekezaji, hatua iliyopongezwa pia na Mbunge wa Newala Vijijini, Dkt. Yahaya Nawanda.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *