• Kiongozi wa Wiper Patriotic Front, Kalonzo Musyoka, amezindua Paybill ya M-Pesa ili Wakenya wachangie kampeni yake ya urais ya mwaka 2027
  • Uzinduzi wa Paybill hiyo umefanyika saa chache baada ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuzindua njia kama hiyo ya michango kupitia vuguvugu lake la Linda Mwananchi
  • Kampeni ya Komboa Kenya inamlenga Kalonzo kama mmoja wa wagombea wakuu wa upinzani dhidi ya Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027

Kiongozi wa Wiper Patriotic Front, Kalonzo Musyoka, amefungua njia ya kuchangisha fedha kutoka kwa umma, akiwaomba Wakenya wachangie kifedha kampeni yake ya urais ya mwaka 2027 kupitia M-Pesa na tovuti maalumu ya michango.

Kalonzo Musyoka
Wiper ya Kalonzo Musyoka imetoa wito kwa Wakenya kuchangia azma yake ya urais 2027. Picha: Kalonzo Musyoka.
Source: Facebook

Tangazo hilo lilitolewa kupitia ukurasa rasmi wa Facebook wa chama hicho, ambapo wafuasi walielekezwa kutembelea stephenkalonzomusyoka.com/donate au kutuma fedha kupitia M-Pesa Paybill Nambari 400200, wakitumia Nambari ya Akaunti 728282 chini ya jina la akaunti Hon. Stephen Kalonzo Musyoka.

Harakati ya Komboa Kenya yawahimiza Wakenya wa kawaida

Pia soma

Edwin Sifuna Akusanya KSh 500k Saa 12 Tu Baada ya Kuzindua Paybill ya Kusaidia Kampeni Yake

Katika ujumbe wake kwa wafuasi, Wiper Patriotic Front ilieleza kuwa zoezi hilo la kuchangisha fedha ni harakati ya kiraia badala ya kampeni ya kawaida ya kisiasa.

“Nchi hii haitabadilika hadi wananchi wake waamue kuimiliki. Kenya si mali ya wanasiasa. Ni mali yako. Sauti yako, juhudi zako na mchango wako ndivyo vitaamua kesho itakuwaje. Kama tunataka Kenya bora, lazima tuache kusubiri na tuanze kuijenga sisi wenyewe. Chukua hatua. Kubali wajibu. Wekeza katika mustakabali unaotaka kuishi. Hii si kampeni tu; ni mwito kwa kila Mkenya kusimama, kuchangia na kushika hatamu ya hatima yetu,” chama hicho kiliandika.

Chama hicho kiliongeza kuwa michango kutoka kwa Wakenya wa kawaida ni uthibitisho kuwa mustakabali wa taifa unaweza kujengwa na raia waaminifu badala ya makundi yenye maslahi binafsi au mitandao ya ufisadi.

Kalonzo, mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Makamu wa Rais, anatafuta kumng’atua Rais William Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2027 kupitia bendera ya Komboa Kenya.

Tovuti ya Kalonzo Musyoka
Picha ya skrini ya tovuti ya Kalonzo Musyoka ikiwaalika Wakenya kutoa michango. Picha: Kalonzo Musyoka.
Source: UGC

Sifuna alizindua Paybill kama hiyo saa chache kabla

Hatua ya Kalonzo imejiri saa chache baada ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuzindua mpango unaofanana wa kuchangisha fedha.

Pia soma

Magazetini: Hasira za walimu zafumuka baada ya nyongeza ya mishahara ya KSh 8.4 bilioni

Kupitia vuguvugu lake la Linda Mwananchi, Sifuna amejiweka kama mmoja wa viongozi wa upinzani wanaotarajiwa kumenyana na Ruto katika uchaguzi wa mwaka 2027.

Kufikia mwisho wa Jumanne, Julai 21, Paybill ya Sifuna ilikuwa tayari imevutia zaidi ya KSh 500,000 kutoka kwa michango ya umma, jambo linaloashiria hamasa kubwa miongoni mwa Wakenya ya kufadhili viongozi wa upinzani kupitia michango ya wananchi kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *