Nchini Sudan, raia wasioupungua 22 wanaripotiwa kuuawa katika mashambulio yanayoaminiwa kutekelezwa na wapiganaji wa RSF katika mji wa kimkakati jimboni Kordofan Kaskazini.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mji wa Rahad ulio kusini mashariki mwa mji mkuu wa jimbo hilo El-Obeid, katika siku za hivi karibuni umekumbwa na mashmbulizi ya droni na ardhini, pamoja na uporaji katika vijiji vilivyo karibu.

Kulingana na vyanzo, raia 16 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa Jumapili iliopita katika Kijiji cha Al Musalamiya kusini mwa mji huo.

Mkanda wa video unaosambaa mitandaoni unaowaonesha wapiganaji wa RSF wakisheherekea mbele ya bango lililoandikwa,“Kituo cha Afya cha Jirani ya Al-Musallamiya”.

Aidha, raia wengine sita waliuawa siku hiyo ya jumapili na wengine 27 kujeruhiwa katika mashambulio ya droni katika soko kuu katika mji huo wa Rahad nae neo lililo karibu la makazi ya watu.

Kulengwa kwa mji wa Rahad kutaiwezesha RSF kulemaza usamabazaji wa vifaa Kwenda katika mji wa El Obeid ambao kwa sasa uko mikononi mwa jeshi la Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *