Mahakama nchini Angola, imewahukumu raia wawili wa Urusi miaka 11 jela, baada ya kupatikana na hatia ya ugaidi na kufanya kazi za kijasusi kinyume cha sheria, wakati wa machafuko yaliyotokea katika nchi hiyo mwaka uliopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maandamano makubwa na kukumbwa  na fujo yaliyotokea kati ya Julai 28 na 30 mwaka uliopita, yaliyopangwa na madereva wa teksi kulalamikia kupanda kwa bei ya mafuta, raia hao wa kigeni wanadaiwa kuhusika kwa kuyaratibu.

Mahakama imekubaliana na viongozi wa mashtaka kuwa, raia hao wa Urusi walichochea maandamano hayo kwa lengo la kutikisa Angola kisiasa na kiuchumi, ili kuipindua serikali na kudhibiti miundo mbinu ya kiuchumi.

Hata hivyo,  raia hao wa Urusi Lev Lakshtanov na  Igor Ratchin, wamekanusha shutuma dhidi yao na kueleza kuwa walikuwa nchini Angola kwa shughuli za kitamaduni na kibiashara.

Maandamano hayo makubwa, yalisababisha vifo vya watu 22, kuwajeruhi wegine zaidi ya 200 huku wengine zaidi ya 1,200 wakikamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *