
Shirika la afya la Umoja wa Afrika (Africa CDC) linaiomba Marekani kuondoa vikwazo vya usafiri dhidi ya Uganda. Hakuna visa vipya vilivyorekodiwa nchini Uganda tangu Juni 21, na mgonjwa wa mwisho aliruhusiwa kutoka hospitalini wiki iliyopita. Kulingana na Africa CDC , kuiweka Uganda kwenye orodha ya nchi zilizoathiriwa haikubaliki tena.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Badala ya ya kuzuiwa kwa kuingia kwa jumla nchini Marekani, Africa CDC inapendekeza hatua zinazolengwa: uchunguzi wa wasafiri wanapoondoka na kuwasili, dodoso za afya, na ufuatiliaji wa haraka wa watu wanaoonyesha dalili za ugojwa huo.
Shirika hilo linategemea uamuzi wake kwa sehemu kukamilika kwa ufuatiliaji kwa watu 836 waliotambuliwa kama watu waliotangamana na wagonjwa wa Ebola. Mgonjwa wa mwisho, ambaye alipimwa na kupatikana hana virusi mara mbili, aliruhusiwa kuondoka hospitalini Julai 16, na Kampala inadai kuwa haina visa vingine.
Hata hivyo, Washington iliongeza muda wa wasafiri kutoka Uganda kuzuiwa Julai 13 kwa siku zingine 30. Jean Kaseya, katika barua kwa Waziri wa Afya wa Marekani, anaona hatua hii kuwa isiyo sawa.
Hata hivyo, Uganda inadumisha ufuatiliaji wa hali ya juu, hasa kando ya mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo mlipuko huo bado unaendelea.
Nchi kuungwa mkono badala ya kuwatengwa
Kwa upande mwingine, mlipuko wa Uganda bado haujamalizika rasmi: nchi lazima isubiri siku 42 kabla ya kutangaza kumalizika wa mlipuko huo. Lakini kwa upande wa Jean Kaseya, nchi zinazogundua haraka milipuko, kuiripoti kwa uwazi, na kujibu kwa ufanisi zinapaswa kuungwa mkono, sio kutengwa.
Ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya watu 1,001 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda, kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa siku ya Jumatano na Shirika la Afya Duniani (WHO), ambalo linategemea data kutoka kwa mamlaka za afya za Kongo. Jumla ya vifo 999 na wagonjwa 2,473 waliothibitishwa wamerekodiwa nchini DRC tangu kuanza kwa janga hilo, lililotangazwa katikati ya mwezi Mei, WHO ilibainisha katika ripoti ya hali ya tarehe 20 Julai.
Ebola, ambayo huambukizwa kupitia kugusana na majimaji ya mwili na husababisha homa ya kutokwa na damu, imeua zaidi ya watu 15,000 barani Afrika katika kipindi cha miaka 50 iliyopita. Mlipuko huo mbaya zaidi nchini DRC umesababisha vifo karibu 2,300 kati ya wagonjwa 3,500 waliorekodiwa, kati ya mwaka 2018 na 2020.