Nani atamrithi Antonio Guteress kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ? Mchakato wa kumtafuta mrithi wake umeanza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kuna wagombea sita, wenye sifa kubwa na wanadiplomasia wakongwe duniani. Macky Sall, rais wa zamani wa Senegal ndio mwafrika pekee kwenye kinyangiro hicho.
Wagombe wanaosalia wanatokea katika bara la Amerika Kusini, ni pamoja na Michelle Bachelet rais wa zamani wa Chile na aliyewahi kuwa Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu.
Maria Fernanda Espinosa Garcés, rais wa zamani wa Umoja wa Mataifa na Waziri wa Mambo ya nje wa Ecuador.
Wengine ni Rafael Mariano Grossi raia wa Argentina, amekuwa Mkuu wa shirika la Kimataifa linaloshughulikia nishati ya Atomiki, Rebeca Grynspan Mayufis kutoka Costa Rica, Katibu Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia biashara na maendeleo na Carolyn Rodrigues Birkett Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Guyana, ambaye pia alikuwa balozi wa nchi yake kwenye Umoja wa Mataifa.
Mrithi wa Antonio Guteress huenda atafahamika Septemba au mwisho wa mwaka huu.