Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Marekani imetangaza kuwa itaongeza ushuru mpya wa forodha wa asilimia 60 kwa washirika wake wa kibiashara, kwa madai kuwa yameshindwa kumaliza utumwa kazini.

Wachambuzi wanasema utawala wa Trump unaendelea kutumia nyongeza ya ushuru wa forodha kama njia ya kuongeza ushawishi wake katika mazungumzo ya kibiashara na mataifa mengine.

Mwanasheria wa biashara Greta Peisch amesema hatua ya kuweka ushuru wa msingi huku ukihifadhi uwezekano wa kuongeza ushuru inaipa Marekani nguvu ya kushinikiza washirika wake kutekeleza makubaliano ya Kibiashara waliyoingia.

Peisch amesema maafisa wa Marekani wanatumia muda kufanya uchunguzi ili kuhakikisha ushuru mpya una msingi imara wa kisheria iwapo utapingwa mahakamani.

Josh Lipsky kutoka Baraza la Atlantic amesema sera hizo zinaashiria kuwa uchumi mkubwa zaidi duniani unaelekea katika msimamo mkali zaidi wa kulinda soko la ndani.

Hatua hizo zimekuja muda mfupi baada ya ushuru wa asilimia 25 kuanza kutumika kwa bidhaa mbalimbali kutoka Brazil, huku Washington ikiishutumu nchi hiyo kwa kufanya biashara isiyo ya haki.

Wiki hii pia Trump alitangaza ushuru mpya wa asilimia 50 kwa bidhaa nyingi kutoka Canada, akidai Ottawa imekuwa ikizibagua bidhaa za Marekani, zikiwemo pombe, magari na bidhaa za maziwa.

Umoja wa Ulaya, ambao tayari umefikia makubaliano ya biashara na Marekani, umeeleza matarajio yake kuwa Washington itaheshimu ahadi zote zilizowekwa katika taarifa ya pamoja kati ya pande hizo mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *