Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani mkazi wa Nanyanje manispaa ya Lindi, Rashid Mohamed Mtala (33) baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya ya Lindi, Muyonga Bugendako Magara baada ya mahakama kujiridhisha kuwa upande wa mashtaka umethibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa pasipo kuacha shaka.
Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa Mahakamani, Rashidi alikamatwa Machi 5, 2026, majira ya saa 11:45 jioni katika eneo la Muhimbili, Barabara ya Jangwani, Wilaya ya Lindi, na askari waliokuwa doria akiwa amehifadhi misokoto 1,511 ya bangi yenye uzito wa kilogramu 1.26, iliyokuwa imewekwa ndani ya mifuko miwili tofauti.�
Mshtakiwa alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Mei 20, 2026 na kusomewa shtaka linalomkabili ambalo alikana.��Katika usikilizwaji wa shauri hilo, upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi sita na vielelezo vinne vilivyoiwezesha mahakama kufikia uamuzi wa kumtia hatiani.
Upande wa mashtaka uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Hilali Hamza.��Taarifa ya Omary Mikoma.��
Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)